Alhamisi 26 Juni 2025 - 08:32
Watu wa Iran ni alama ya nguvu na heshima ya ulimwengu wa Kiislamu

Hawza/ Hujjatul-Islam Haj Rahid Karim, Imamu wa Ijumaa wa Msikiti wa Ahlul Bayt katika eneo la Soghanliq, mji wa Tbilisi, alisema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi anasema: "Sisi ni wenye kudhulumiwa, lakini si dhaifu." Hivi sasa dunia inashuhudia vita katika medani mbili: upande mmoja wapo Mayahudi, na upande mwingine wapo Waislamu. Upande mmoja ni wajenzi wa ngome ya Khaybar, na upande mwingine wamesimama washindi wa Khaybar.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, likinukuu kutoka katika Umoja wa Redio na Televisheni za Kiislamu, Hujjatul-Islam Haj Rahid Karim, Imamu wa Ijumaa wa Msikiti wa Ahlul Bayt katika eneo la Soghanliq, mji wa Teflisi, ameeleza kuwa; leo hii watu wa Iran ni fahari kwa Mashia na kwa ulimwengu wa Kiislamu, alisema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi anasema: "Sisi ni wenye kudhulimiwa, lakini si dhaifu." Hivi sasa dunia inashuhudia vita katika pande mbili: upande mmoja wapo Mayahudi, na upande mwingine wapo Waislamu. Upande mmoja ni wajenzi wa ngome ya Khaybar, na upande mwingine wamesimama washindi wa Khaybar.

Akaongeza kuwa: Katika zama zilizopita, ambapo jamii ya Kiislamu, hasa jamii ya Kishia, ilikuwa haina uongozi wa hekima na busara, watu walikuwa wakiuliza: je, Shia ina asili halisi au la? Je, Shia imetokea wapi? Lakini sasa tumefikia mahali ambapo nchi yenye nguvu zaidi miongoni mwa Waislamu ni ya Mashia, kwa sababu nchi hii na njia hii imo katika njia ya Mtume na Ali na Husein (as)

Imamu wa Ijumaa wa mji wa Teflisi aliendelea kusema kwamba: Tunajivunia kwamba kuna nchi ya Kiislamu ambayo imeukamata uso wa yule anayedhaniwa kuwa shujaa miongoni mwa Mayahudi na ikamuangamiza, na ikawapa Waislamu heshima. Naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa; Ayatollah Khamenei ni fahari na heshima yetu. Je, ni wapi mnaweza kuona nchi yoyote inayothubutu kukabiliana na Israel?

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha